MANCHESTER UNITED YASITAKIWA NA FA.
Refa Michael Oliver alizungukwa na wachezaji wa United baada ya kumpa kadi nyekundu Ander Herrera dakika 10 kabla ya muda wa mapumziko ambapo United ilipoteza mechi hiyo kwa 1-0.
Taarifa ya FA ilisema kuwa United ina hadi saa kumi na mbili jioni saa za Uingereza kujibu.
Kiungo wa kati wa Uhispania Herrera alitolewa nje baada ya kumchezea visivyo kwa mara ya pili mshambuliaji Eden Hazard.
Hakuna hatua zaidi itakayochukuliwa dhidi ya Marcos Rojo baada ya kisa alichofanya katika dakika za mwisho za mechi ambapo Rojo alionekana akimkanyaga Hazard.
0 comments: