JUVENTUS YAILAZA PORTO CHAMPIONS LEAGUE.
Juventus imefanikiwa kuingia robo fainali ya Klabu Bingwa Ulaya kwa kuilaza Porto bao 1-0.
Paulo Dyabala alifunga bao hilo pekee kwa mkwaju wa penati kufuatia Pereira kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.

Pereira alitolewa nje kwa kadi nyekundu.
Droo ya robo fainali itafanyika siku ya Ijumaa Machi 17.
0 comments: