LEICESTER CITY YATINGA ROBO FAINALI CHAMPIONS LEAGUE.

Leicester City wameifunga Sevilla magoli 2-0 na kuingia robo fainali ya Klabu Bingwa Ulaya, kwa jumla ya magoli 3-2 katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa King Power.
Nahodha wa Leicester Wes Morgan alipachika bao la kwanza katika dakika ya 27, na kufanya matokeo kuwa ya sare ya 2-2 dhidi ya Sevilla ambao walionekana kutocheza kwa kuelewana.
Marc Albrighton alifunga goli muhimu la pili mapema katika kipindi cha pili, kabla ya kiungo Samir Nasri kuoneshwa kadi ya pili ya manjano na kutolewa nje.
Licha ya kucheza pungufu, Sevilla walipoteza nafasi ya kuupeleka mchezo katika muda wa ziada baada ya Kasper Schmeichel kuokoa mkwaju wa penati uliopigwa na Steven Nzonzi.
Droo ya robo fainali itafanyika siku ya Ijumaa Machi 17.

0 comments: