Feature news

SAMATTA AISAIDIA KRC GENK KUINGIA ROBO FAINALI EUROPA LEAGUE.

Samatta
Mchezaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta aliisaidia timu yake kuingia robo fainali ya michuano ya UEFA Europa League dhidi ya KAA Gent licha ya mchezo huo kumalizika kwa sare ya 1-1.

Samatta alipachika mabao mawili katika mchezo wa awali na hivyo KRC Genk kusonga mbele kwa jumla ya mabao 6-3.

MATOKEO MENGINE
Besitkas imeingia robo fainali kwa jumla ya mabao 5-2 dhidi ya Olympiakos, Celta Vigo ilishinda 4-1 dhidi ya FK Krasnodar, Ajax imeishinda FC Copenhagen kwa 3-2, FC Schlake imesonga mbele kwa magoli ya ugenini dhidi ya Borussia Monchengladbach katika mechi mbili zilizomalizika kwa 3-3. Roma ya Italia iliweza kuingia robo fainali kwa kuichapa Lyon kwa jumla ya magoli 5-4 na Anderlecht kusonga mbele kwa 2-0 dhodo ya Apoel Nicosia.


Droo ya Klabu Bingwa Ulaya na Europa League itafanyika Ijumaa Machi 17.
Learn more »

MANCHESTER UNITED YASONGA MBELE EUROPA LEAGUE.

Manchester United wamesonga mbele na kuingia robo fainali ya michuano ya UEFA Europa League baada ya kuifunga Rostov 1-0 katika mchezo wa raundi ya pili uliochezwa Old Trafford. 

United wamesonga mbele kwa jumla ya magoli 2-1.

Juan mata ndio alifunga bao hilo pekee katika mchezo ambao United walionekana kupata tabu kuvunja ngome ya Rostov. Manchester United wangeweza kusonga mbele hata kwa matokeo ya 0-0 kwa kuwa tayari walikuwa na goli la ugenini.

Wasiwasi kwa mashabiki wa Manchester United pengine ni kuumia kwa kiungo wao Paul Pogba ambaye hakumaliza mchezo, kutokana na kuumia msuli wa paja. Nafasi yake ilichukuliwa na Marouane Fellaini.

United walitawala mpira lakini hawakufanikiwa kupata chochote hadi katika dakika ya 70 ambapo Mata alifunga bao hilo la ushindi.
Learn more »

SIMBA YAIHOFIA MADINI FC YA ARUSHA, YAIFANYI MAZOEZI MARA MBILI KWA SIKU.


Kikosi cha Simba kilicho mjini Arusha, kitafanya mazoezi mara mbili kwa siku ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho dhidi ya Madini FC.

Simba itaivaa Madini FC ya Arusha katika mechi ya Kombe la Shirikisho itakayochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Jumapili hii.

Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja amesema hawataidharau Madini kwa kuwa hayo ni mashindano na wanajiandaa kwa umakini mkubwa.

“Mazoezi yatakuwa mara mbili kwa siku, hii ni sehemu ya maandalizi. Hii inategemea na programu yetu, wakati mwingine mara moja kwa siku,” alisema Mayanja.
Learn more »

HIZI NDIZO TIMU ZILIZOINGIA CHAMPIONS LEAGUE.

Nchi zilizovusha timu 8 katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ni nne tu.

Hispania ndiyo imetawala zaidi kwa kuvusha timu tatu, ikifuatiwa na Ujerumani yenye mbili wakati Italia, Ufaransa, England na Italia zimevusha moja kila moja.

Real Madrid ya Hispania ndiyo mabingwa watetezi na wanaongoza kulitwaa mara nyingi zaidi.

HISPANIA:
Real Madrid, Barcelona, Atletico Madrid

UJERUMANI
Bayern Munich, Borussia Dortmund

ENGLAND:
Leicester

UFARANSA:
Monaco

ITALIA:
Juventus
Learn more »

YANGA KUIFATA ZANACO BILA TAMBWE NA NGOMA.

Image may contain: one or more people, stadium, grass and outdoor
WASHAMBULIAJI wote tegemeo wa Yanga, Mrundi Amissi Joselyn Tambwe na Mzimbabwe Donald Dombo Ngoma hawatasafiri na timu kesho kwenda Zambia kwa mchezo wa marudiano na wenyeji, Zanaco hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika.

Tambwe hakucheza kabisa mechi ya kwanza dhidi ya Zanaco Jumamosi ya Machi 11, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Ngoma alijitonesha goti katika mchezo huo baada ya kurejea kufuatia kuwa nje tangu Janauri.

Katibu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema leo mjini Dar es Salaam kwamba pamoja na wawili hao ambao ni majeruhi, pia klabu itawakosa kipa Beno Kakolanya, beki Pato Ngonyani, kiungo Yussuf Mhilu na washambuliaji wengine wawili, wote wazawa, Malimi Busungu na Matheo Anthony ambao pia ni wagonjwa.

Mkwasa amesema wachezaji 20 tu ndiyo watasafari na timu kesho kwa ndege ya Shirika la Kenya kwenda Lusaka kwa ajili ya mchezo huo wa Jumamosi na kwa bahati mbaya hakutakuwa na mshambuliaji halisi hata mmoja.

Hawa ni makipa; Deogratius Munishi ‘Dida’ na Ally Mustafa ‘Barthez’, mabeki ni Oscar Joshua, Mwinyi Hajji Mngwali, Hassan Kessy, Juma Abdul, Vincent Bossou, Andrew Vincent ‘Dante’, Kevin Yondan na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’.

Viungo ni Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Justine Zulu, Said Juma ‘Makapu’, Juma Mahadhi, Simon Msuva, Geoffrey Mwashiuya, Obrey Chirwa na Emanuel Martin. 

Yanga inahitaji ushindi wa ugenini Jumamosi ili kwenda hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 Jumamosi iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Learn more »

WANASHERIA WA MANJI WAWASILISHA MAOMBI APANDISHWE KIZIMBANI ISHU YA UHAMIAJI


Wakati Mwenyekiti wa klabu ya mpira ya Yanga, Yusuf Manji anapanda tena Mahakama ya Kisutu kujibu kesi ya tuhuma za madawa ya kulevya, wanasheria wake wamesilisha hati ya maombi kutaka apandishwe kizimbani kwa kesi ya uhamiaji.

Taarifa zinaeleza, wanasheria wa Manji wamewasilisha hati hiyo mahakamani wakitaka apandishwe mahakamani kwa kesi ya uhamiaji ambao wanamtuhumu kuingia nchini kinyume na sheria.

Manji amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan lakini chini ya ulinzi wa Maofisa wa Uhamiaji pamoja Jeshi la Polisi.

Hata hivyo kwa zaidi ya wiki tatu sasa, hajawahi kupandishwa kizimbani. Hali iliyosababisha wanasheria wake kuwasilisha hati hiyo ya maombi.
Learn more »

MYWEATHER KUZICHAPA NA MCGREGOR KWA DAU LA BILLION 200.


Mabondia Floyd Mayweather na Conor McGregor watapanda ulingoni Juni 10, mwaka huu wameuteua ukumbi wa T-Mobile Arena mjini Las Vegas kuwa shehemu ya pambano lao.

Kila mmoja ametaja bei yake ya kupandia ulingoni kuwa dola za Kimarekani Milioni 100, ila kiuhalisia bondia McGregor atatakiwa kushusha bei ili kuhamishia ujuzi wake wa UFC katika ndondi.

Mayweather amesema rasmi amerejea ulingoni kwa ajili ya McGregor baada ya kustaafu akiwa amepigana mapambano 49 na kushinda yote rekodi sawa na ya gwiji, legendary Rocky Marciano na hilo litaitwa “Pambano la Karne”.
Learn more »